Jumapili 13 Julai 2025 - 23:06
Zaidi ya mafakihi na walimu 400 wa Hawza ya Qom waiunga mkono kikamilifu fatwa ya kihistoria ya maraaji’ wa taqlid

Hawza/ Zaidi ya watu 400 miongoni mwao ni mafakihi na walimu wanachama wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom "J'amiat Mudarisin" wametangaza uungaji mkono wao wa wazi na wa dhati kwa fatwa ya maraaji’ wa taqlid, kuhusiana na hukumu ya kuwa “muharib” wale wanaotoa vitisho dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi na taasisi ya marjaiyyah.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, fuatilia tamko la uungaji mkono wa wazi na thabiti la zaidi ya mafakihi na walimu 400 wanachama wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom kwa fatwa ya maraaji’ wa taqlid (zidumu baraka zao) kuhusu hukumu ya kuwa muharib wale wanaotoa vitisho dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi Ayatollah al-Udhma Imam Khamenei (Mola amuhifadhi) na marjaiyyah ya kidini:

بسم الله الرحمن الرحیم

وَأَعِدُّوا لَهُم مَّا اسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ
وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ
وَقَاتِلُوا أَئِمَّةَ الْكُفْرِ

Katika zama ambazo ukafiri wote umesimama dhidi ya Uislamu wote, ukiwa na azma ya kuubomoa na kuuondoa Uislamu mtukufu, huku wakiwasha moto wa damu dhidi ya Waislamu wa Ghaza kwa miaka mingi, na vilio vya wanyonge wa Kiislamu vinasikika duniani kote hivi sasa, kwa ujasiri na uovu zaidi kuliko wakati wowote, wameonyesha makucha yao dhidi ya kituo cha Uislamu na dini, na kwa kiburi kisicho kifani, wameanzisha mashambulizi dhidi ya marjaiyyah ya Kiislamu, ambayo ni alama za heshima na kinga ya Waislamu, na wamefikia hadi hatua ya kutoa vitisho vya moja kwa moja kwa nafsi tukufu ya marjaiyyah na uongozi wa ulimwengu wa Kiislamu, yaani Ayatollah al-Udhma Imam Khamenei (Mola amuhifadhi).

Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom, inalaani kwa ukali tendo hili ovu ambalo ni dhihirisho la wazi la kuutukana Uislamu, vitu vitakatatifu vyake, na Waislamu wa dunia nzima, imetangaza kuunga mkono kwa dhati fatwa hiyo nyeti, ya kihistoria, na yenye ujasiri ya maraaji’ wa taqlid wa Qom na Najaf Ashraf (zidumu baraka zao), ambayo imewahukumu kuwa muharib wamiliki wa fikra hii ovu, na kuitangaza kuwa ni wajibu kwa Waislamu wote kujitokeza kwa nguvu katika kuwatetea ili wapate majuto makubwa.

Aidha, Jumuiya hii inawaomba watu wote huru na wenye ujasiri, hasa Waislamu duniani kote, kusimama kwa ajili ya kuikomboa jamii ya kibinadamu, kuimarisha heshima na utukufu wa Uislamu, na kuangamiza serikali na tawala za kigaidi za Kizayuni za Israel na Marekani, na kuingia katika jihadi na mapambano dhidi ya utawala huu wa kibaguzi, muuaji wa watoto, wenye damu mikononi mwake, na mdhamini wa jinai – yaani Marekani – ambayo ni tishio kwa ubinadamu na mwanadamu katika dunia nzima.

Walimu wa Jumuiya ya Hawza ya Qom, wamezitaka mahakama za kimataifa kuwafikisha kwenye mikono ya sheria na kuwahukumu Grossi msaliti na jasusi, Netanyahu na Trump kama wahalifu wa kivita, ili haki ya taifa tukufu na lenye nguvu la Iran irejeshwe.

Maafisa na wanajeshi wa Imam wa Zama (aj) wataendelea kuulinda kwa jitihada zote mfumo mtukufu, damu ya mashahidi, na hadhi ya juu ya marjaiyyah hadi pumzi ya mwisho na tone la mwisho la damu, na pamoja na taifa lenye ushindi la Iran, kama walivyoshinda vita vya mseto vya kimataifa vya siku 12 zilizopita, wataikandamiza pua ya uistikbari wa kimataifa na shetani mkubwa Marekani.

اللهم عجل لولیک الفرج
نصر من الله و فتح قریب

Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha